MCHANGA WA DHAHABU

MCHANGA WA DHAHABU.



Salamu muhasibu,kazi yako natambua,
Unazozipata tabu,hata mimi nazijua,
Kazi inakusulubu,pia una familia,
Mambo mengi yakusibu,pole ninakupatia.


Wengi wamekuwa bubu,kwako nimeshasogea,
Najua waweza jibu,maswali nakuletea,
Haya yanayotusibu,hata wewe hukujua?
Eti mchanga dhahabu,mwingi umeshapotea.


Ule mkataba bubu,nawe hukuupitia?
Vipi na makatibu,nao hawakuujua,
Waziri ameshatubu,pengine alisinzia.

Japo tumeshaharibu,kisa ni makanikia.

No comments:

Powered by Blogger.