TUMAINI


TUMAINI
Josephat S. Hema

Hii siku ikiisha,mimi nawe tu washindi,
Tumeyaweza maisha,japo ni vingi vipindi,
Dhoruba itapokwisha,tutauimba ushindi,
Tumaini niko nawe,nawe uko na mimi.

Akufaaye kwa dhiki,kwenye shida na raha,
Huyo ndiye rafiki,usimwache akahaha,
Ni wewe ninaafiki,pekeako unafaa,
Tumaini niko nawe,nawe uko na mimi.

Zilishakuja mvua,na jua la utosisni,
Wote tukakimbia,ila leo naamini,
Mkono hukuuachia,tufe wote dhorubani,
Tumaini niko nawe,nawe uko na mimi.

Wewe nakutegemea,nimeamua kuamini,
Chini wote tutalia,na kicheko furahani,
Name ninakuapia,sitakwacha asilani,
Tumaini niko nawe,nawe uko na mimi.



No comments:

Powered by Blogger.