MTEMBEZI


MTEMBEZI.
Josephat S. Hema



Mtembezi safarini,
Bahasha mkononi,
Kutwa barabarani,
Ametoka chuoni,
Mtaani wafanya nini?

Eti msomi wa chuo,
Mbona huna maendeleo,
Shahada yako sio,
Haina maana leo,
Za sakafuni mbio.
Ukingo ndio kituo.

Mtembezi mtaani,
Mara yuko vijiweni,
Hadithi zake makini,
Kichwa kina madini,
Ila yuko nyumbani.

Haimtaki serikali,
Kwa sasa haiajiri,
Inao watu mahiri,
Anapaswa kusubiri,
Hali mekuwa shubiri.

Mtembezi nchini,
Anaeshinda juani,
Na ujuzi kichwani,
Ila hakai ofisini,
Atafanya nini?

No comments:

Powered by Blogger.