NJIA.

NJIA
Josephat S. Hema


Duniani nimejua,
Ukitaka fanikiwa,
Zipo nyingi njia,
Nazo zinatumiwa.



Ila nimeamua,
Baadhi kuchukua,
Nyingine sitatumia.


Nataka ishika njia,
Ilio sawa sawia,
Nyingine nitajutia,
Hata wakishangilia.


Njia niliyochagua,
Japo ngumu ninajua,
Ila mwisho nakwambia
Sana nitafurahia,
Mede nikiifikia.



No comments:

Powered by Blogger.